Tarehe 25 Machi 2026, jijini Ankara, Mhe. Balozi Iddi Seif Bakari alikutana kwa mazungumzo na Bw. Mohammed İdin, Meneja Mkuu wa Kampuni ya AVES yenye Makao Makuu yake mjini Mersin, Uturuki. Kupitia mazungumzo hayo walijadili na kukubaliana kuendeleza ushirikiano katika sekta za biashara na uwekezaji. Tayari kampuni hiyo imeonesha nia ya kuwekeza nchini Tanzania kwenye kilimo cha alizeti kiwanda cha kuchakata mafuta na mazungumzo yanaendelea kufanikisha azma hiyo. Aidha, Mhe. Balozi Bakari alimuahidi ushirikiano wa Ubalozi katika kuhakikisha miradi hiyo inatekelezwa kwa maslahi ya pande zote mbili.

