Balozi wa Tanzania nchini Uturuki, Mhe. Iddi Seif Bakari, leo Aprili 28, 2026, amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Urusi nchini Uturuki, Mhe. Sergey Vershinin, jijini Ankara. Kupitia mazungumzo hayo, wamejadili masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya Tanzania na Urusi katika sekta ya nishati, utalii na ushirikiano wa uwili katika masuala ya kimataifa kwa lengo la kuimarisha ushirikiano wenye maslahi kwa pande zote mbili.