Mheshimiwa Balozi Iddi Seif Bakari amekutana na kufanya mazungumzo na Ndg. Metin Gümüşçü, Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya AKSOY Group ya nchini Uturuki, tarehe 24 Machi 2026, Ubalozini Jijini Ankara. Mazungumzo hayo yalijadili ushirikiano kwenye sekta ya ujenzi, ambapo kampuni hiyo imeonesha nia ya kushirikiana na Tanzania katika miradi ya ujenzi, hususan katika sekta ya barabara. Kwa muda mrefu Kampuni ya AKSOY Group imekuwa ikishughulisha na miradi ya ujenzi kwenye nchi mbalimbali za Mashariki ya Kati na Afrika.

