Mhe. Balozi Iddi Seif Bakari amekutana na kufanya mazungumzo na Mhe. Didace Ntureka, Balozi wa Burundi nchini Uturuki, Machi 13, 2026, katika Ubalozi wa Tanzania uliopo Jijini Ankara, Uturuki. Kupitia mazungumzo hayo walijadili masuala mbalimbali kuhusu nchi hizi mbili yenye lengo la kuimarisha ushirikiano wa uwili na kikanda kwa manufaa ya pande zote mbili katika nyanja za kisiasa, kiuchumi na kijamii.

  • Balozi wa Tanzania nchini Uturuki Mhe. Iddi Seif Bakari (kulia) akiwa na Balozi wa Burundi nchini Uturuki, Mhe. Didace Ntureka, mara baada ya mazungumzo kukamilika.