Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. January Makamba amewasili Ankara, Uturuki leo tarehe 16 Aprili 2024 na kukutana kwa mazungumzo na mwenyeji wake Waziri wa Mambo ya Nje wa nchi hiyo Mhe. Hakan Fidan.
Pamoja na mambo mengine viongozi hao wamejadili kuhusu kukamilika kwa maandalizi ya ziara ya kitaifa ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan itakayofanyika nchini humo kuanzia tarehe 17 hadi 21 Aprili 2024.
Wakati wa ziara hiyo ambayo inafanyika kufuatia mwaliko wa Rais wa Jamhuri ya Uturuki, Mhe. Recep Tayyip Erdoğan viongozi hao watashuhudia kusainiwa kwa Hati za Makubaliano nane (8) katika sekta za Elimu, Utalii, Utunzaji Kumbukumbu na ushirikiano katika masuala ya Diaspora.