Tarehe 02 Oktoba 2025, Jijini Ankara, Mhe. Balozi Iddi Seif Bakari alifanya mazungumzo na Bw. Deodat Maharaj, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Teknolojia ya Umoja wa Mataifa kwa ajili ya Nchi zenye Uchumi mdogo (LDCs). Katika mazungumzo hayo walijadili mkakati wa Shirika hilo unaolenga kuimarisha matumizi teknolojia nchini Tanzania kwenye sekta za kipaumbele ikiwemo kilimo, biashara na shughuli za uvuvi endelevu hususan kilimo cha mwani nchini ili kukuza ushiriki wa sekta wa sekta binafsi na kuongeza mchango wa sekta hizo kwenye uchumi na kuinua maisha ya wananchi.

