Tanzania imeshiriki Kongamano la Biashara na Uchumi kati ya Uturuki na Afrika (Türkiye - Africa Business and Economic Forum), ambalo limefunguliwa Oktoba 16, 2025, jijini Istanbul na Mhe. Prof. Dkt. Ömer Bolat, Waziri wa Biashara wa Jamhuri ya Uturuki na kuhudhuriwa na Mawaziri, Mabalozi, Viongozi Waandamizi wa Serikali na Sekta binafsi. Ujumbe wa Tanzania kwenye kongamano hilo umeongozwa na Ndg. Asangye N. Bangu, Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Stakabadhi za Ghala (WRRB), akimwakilisha Mhe. Waziri wa Viwanda na Biashara.
Kongamano hilo ambalo litahitimishwa Oktoba 17 2025, litajadili na kuweka mikakati ya pamoja yenye lengo la kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi na kukuza maendeleo ya sekta za biashara na uwekezaji, kilimo, afya, teknolojia na miundombinu.
