Novemba 25, 2025, Mhe. Balozi Iddi Seif Bakari alikutana kwa mazungumzo na Balozi Volkan Işikçi, Mkurugenzi Mkuu wa Kusini mwa Afrika na Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje ya Uturuki. Mazungumzo hayo yalitoa fursa ya kujadili kwa upana masuala ya uwili na walikubaliana kuendelea kuimarisha ushirikiano wa kimkakati katika nyanja za biashara, uwekezaji, na afya. Aidha, Ubalozi utaendelea kutafuta fursa muhimu zenye mchango chanya katika kukuza uchumi wetu ili kuwaletea wananchi maendeleo
