Balozi wa Tanzania nchini Uturuki, Mhe. Iddi Seif Bakari, tarehe 28 Novemba 2025, akiwa kwenye ziara ya kikazi Jijini Istanbul, alikutana na ujumbe wa Tanzania unaohusisha Watendaji na Maafisa Waandamizi wa Serikali ambao upo nchini Uturuki kikazi. Ujumbe huo unaongozwa na Kamishna Msaidizi, Idara ya Usimamizi wa Madeni, Wizara ya Fedha, Bw. Omary Khama.
Kwa upande wake Balozi Bakari aliuhakikishia ujumbe huo dhamira ya Serikali ya kuimarisha ushirikiano na nchi ya Uturuki katika maeneo ya kipaumbele ikiwemo biashara, uwekezaji, afya, na elimu ili kuchochea maendeleo na kukuza uchumi.
