Ubalozi wa Tanzania nchini Uturuki ulishiriki kwenye Mkutano wa Vision'25 Connectivity, ulioandaliwa na Umoja wa Wamiliki wa Viwanda na Wafanyabiashara nchini Uturuki (MÜSIAD), Desemba 2, 2025, jijini Istanbul. Katika mkutano huo Balozi Iddi Seif Bakari alifanya mazungumzo na viongozi wa kampuni na wadau wa biashara nchini Uturuki lengo likiwa ni kuvutia wawekezaji na kunadi maeneo ya kipaumbele katika sekta za biashara na uwekezaji.



