Tarehe 25 Machi 2022, Mhe. Lt. Jen. Y. H. Mohamed, Balozi wa Tanzania nchini Uturuki ametembelea Ofisi za Makao Makuu ya Yapi Merkezi nchini Uturuki na kufanya mazungumzo na Dkt. Ersin Arioglu, Mwenyekiti wa Kampuni ya Yapi Merkezi. Washiriki wengine ni pamoja na Bw. Asian Uzun, Mtendaji Mkuu (CEO) wa Kapuni hiyo na Wakurugenzi wengine.