Tarehe 25 Mei 2025, Mhe. Iddi Seif Bakari, Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Ankara alipokea ujumbe kutoka Chuo cha Taifa cha Ulinzi (NDC-Tanzania), ambao uko nchini Uturuki kwa ziara maalum ya mafunzo. Ujumbe huo wenye jumla ya washiriki 28 unao ongozwa na Brig. Gen. Method Kamugisha Matunda, uliwasili Uturuki tarehe 24 Mei 2025 na utahitimisha ziara yao tarehe 31 Mei 2025. Wakiwa nchini Uturuki, watatembelea Wizara na Taasisi mbalimbali kwa lengo la kujifunza na kubadilishana uzoefu wa masuala mbalimbali kuhusu ushirikiano kisekta hususan ulinzi na uhusiano wa kimataifa.

Kwa upande wake Balozi Iddi aliipongeza NDC kwa kuichagua Uturuki kama nchi ya kimkakati kwa ajili ya kufanya mafunzo yao pamoja na kutenga muda wao kutembelea Ubalozi. Aidha, alisifu ushirikiano mzuri uliopo kati ya Tanzania na Uturuki ambapo nchi hizi mbili zinashirikiana kwenye maeneo mbalimbali ikiwemo mafunzo kwa maslahi ya pande zote mbili.

Hafla hiyo ilihudhuriwa pia na Waambata Jeshi kutoka nchi za Rwanda, India, Bangladesh na Nigeria.