Mhe. Lt. Jen. Y. H. Mohamed, Balozi wa Tanzania nchini Uturuki ametembelea Ofisi ya Mwakilishi wa Heshima wa Tanzania kwenye jiji la Istanbul, Bw. Ziya Karahan tarehe 26 Machi 2022. Kwenye mazungumzo yao wamekubaliana kushirikiana zaidi katika kutekeleza  na kuimarisha diplomasia ya uchumi.