Tarehe 20 Machi 2025, Mhe. Iddi Seif Bakari, Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Uturuki, amekutana kwa mazungumzo na Bw. Mustafa Efe, Mkuu wa Uhusiano wa Kimataifa katika Baraza la Elimu ya Juu (Council of Higher Education) la Uturuki. Kupitia mazungumzo hayo wamekubaliana kuimarisha ushirikiano wa kimkakati katika kuendeleza elimu ya juu kati ya Tanzania na Uturuki, pamoja na dhamira ya kufungua maeneo mapya ya ushirikiano ili kukuza sekta ya elimu kwa maslahi ya pande zote mbili.