Tarehe 25 Machi 2025, Mhe. Iddi Seif Bakari, Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Uturuki, amepokea ugeni wa Bi. Nighat Tanol, Mkurugenzi kutoka Chuo Kikuu cha Bahçeşehir (BAU). Chuo hicho kina matawi ( campuses ) katika nchi za Uturuki, Ujerumani, Marekani, Georgia na Jamhuri ya Uturuki ya Cyprus Kaskazini. Mkurugenzi huyo alifika Ubalozini kwa lengo la kuelezea shughuli za kitaaluma zinazoendeshwa na Chuo hicho, fursa za elimu pamoja na dhamira ya kuimarisha ushirikiano katika sekta ya elimu na vyuo vikuu nchini Tanzania.