Maonyesho ya Kimataifa ya Zana za Kilimo - Konya Agriculture Fair 2023 yameziduliwa leo mjini Konya Uturuki. Mhe. Lt Jen Yacoub Hassan Muhamed, Balozi wa Tanzania nchini Uturuki na Mhe. Leonard N. Boyo, Balozi wa Kenya nchini Uturuki wameshiriki kwenye maonyesho hayo kufuatia mualiko rasmi kutoka kwa waandaaji.
Manyesho hayo yatafanyika kuanzia tarehe 14-18 Machi 2023. Makampuni zaidi ya 365 kutoka Uturuki, Ulaya na Asia yanaonesha zana mbalimbali za kilimo.