Mhe. Iddi Seif Bakari, Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Nchini Uturuki akiwa kwenye picha ya pamoja na Maafisa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ambao walitembelea Ubalozini. Maafisa hawa wamekuja nchini Uturuki kuhudhuria mafunzo ya muda mfupi katika Chuo cha Diplomasia cha Wizara ya Mambo ya Nje Uturuki, kuanzia tarehe 03 – 09 Februari, 2025.