Mhe. Iddi Seif Bakari, Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Uturuki, tarehe 17 Januari, 2025 alikutana na Menejimenti ya Kiwanda cha Aves kilichopo mji wa Mersin kwa lengo la kufanya mazungumzo kwa ajili ya kuuza Mafuta ya Alizeti pamoja na kufanya uwekezaji wa kulima na kujenga kiwanda cha kuchakata Mafuta ya Alizeti nchini Tanzania.