Mhe. Iddi Seif Bakari, Balozi wa Tanzania nchini Uturuki amefanya mazungumzo na Ndg. Cansel Cevikol Tuncer, Katibu Mkuu wa Manispaa ya Jiji la Antalya tarehe 30.01.2024. Pamoja na mambo mengine wawili hao walikubaliana kushirikiana kwenye sekta mbalimbali ikiwemo Utalii.